Kileleni raha nyie!

KAGERA: Timu ya Simba imeibuka ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Kagera Sugar , kuwarejesha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mchezo uliochezwa uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Mabao ya Simba yamefungwa na beki wa kulia, Shomari Kapombe dakika ya 13 akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na beki wa kushoto wa wekundu hao wa Msimbazi, Mohammed Hussein.La pili kwa Simba limefungwa na Charles Ahoua mpira wa faulo baada ya kuchezwa madhambi na mchezaji wa Kagera Sugar.
Bao la tatu la Wekundu hao wa Msimbazi limefungwa dakika ya 54 na Fabrice Ngoma akiunganisha kona iliyopigwa na Ladack Chasambi, Steven Mukwala aipatia Simba bao la nne na tano baada ya kazi nzuri ya Chasambi.
Kagera Sugar wamepata bao la kwanza dakika ya 80 limefungwa na Datius Peter bao la pili limefungwa na Clephonce Mkandala dakika ya 93.
Kwa ushindi huo Simba inayonolewa na Kocha Fadlu Davids amefikisha pointi 34 katika michezo 13 ikimshusha Azam FC hadi nafasi ya pili ikiwa na alama 33 ambayo imecheza michezo miwili zaidi.
Upande wa Kagera Sugar chini ya kocha Melis Medo wapo katika hali mbaya wakikamilisha michezo 15 ya mzunguko wa kwanza ikiwa na alama 11.