Ligi KuuNyumbani

Mambo 3 kutatua mgogoro wa Feisal, Yanga

MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga imesema imempa machaguo matatu mchezaji wake kiungo Feisal Salum ‘Feitoto’ ili kumaliza mgogoro unaoendelea kati ya pande hizo mbili.

Rais wa Yanga Mhandisi Hersi Said

 

Rais wa Yanga Mhandisi Hersi Said amesema hayo Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizungumza kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM.

“Tumempa Feisal machaguo matatu. 1. Arudi kutumikia mkataba wake, 2. Kama tatizo ni maslahi aje tuzungumze kwa sababu upande wa Yanga hatuna shida na kumboreshea maslahi yake, 3. Klabu yoyote inayomtaka Feisal ije tuzungumze nayo sisi kama Yanga hatuna shida,”amesema Hersi.

Hersi amefafanua kuwa Feisal hakuwa na tabia ya utovu wa nidhamu klabuni hapo na klabu inaendelea kumlipa mshahara kama kawaida.

Yanga imekuwa na mgogoro na mchezaji wake Feitoto unaolezwa kuwa wa kimaslahi hali iliyomfanya Feitoto kuwasilisha maombi ya kutaka kuvunja mkataba na klabu hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button