Ligi Kuu

Azam FC kuweka kambi nje ya nchi

DAR ES SALAAM: UONGOZI wa Azam FC umesema uko katika mipango ya kuhakikisha kikosi cha timu hiyo kinaweka kambi nje ya nchi kipindi ambacho Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi na CHAN.

Msemaji wa Azam FC, Hashim Ibwe amesema wamepata mialiko Afrika Kusini,  Zambia, Qatar na Dubai kati ya nchi hizo wanaangalia nchi gani kwao ina manufaa kwa ajili ya kuajiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.

“Wachezaji wamepewa mapumziko mafupi na viongozi wanaangalia katika mialiko tuliyopata ni nchi ipi wataridhia na inatija kwetu na kwenda kuweka kambi kwa kipindi chote,” amesema.

Ibwe amesema kipindi cha mapumziko ya ligi hiyo kocha Rachid Taoussi amepanga kucheza mechi tatu hadi nne za kirafiki kwa ajili ya kujiimarisha zaidi.

“Mechi hizo zitawapa nafasi ya wachezaji ambao hawakupata nafasi ya kucheza duru la kwanza lakini pia walikuwa na  majeraha nao waweze kupata mechi za ushindani kujenga utimamu wa mwili,” amesema Ibwe.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button