Ligi KuuNyumbani

Mtibwa Sugar kuzinduka kwa Mashujaa leo?

BAADA ya kupokea kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Yanga katika mchezo pekee wa Ligi Kuu Tanzania Bara Desemba 16, Mtibwa Sugar leo inashuka uwanja wake wa Manungu, Morogoro kuikabili Mashujaa.

Mtibwa inashika nafasi ya 16 mwisho wa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 13 wakati mashujaa ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 9 baada ya michezo 11.

Katika michezo miwili ya ligi hiyo iliyofanyika Desemba 18 Dodoma Jiji imeutumia vizuri wake wa nyumbani wa Jamhuri, Dodoma kwa kupata ushindi wa bao 1-0.

Nayo Coastal Union imepata ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya JKT Tanzania kwenye uwanja wa Azam Complex.

Related Articles

Back to top button