Burudani

Kiba atajwa NXT Honor

MSANII wa Bongo Fleva Ali Kiba, ‘King Kiba’ ametangazwa rasmi na NXT Honor kutoka nchini Nigeria kuwa mshindi wa Tuzo ya Heshima ya Maisha ya 2024, na kumfanya kuwa mtu wa kwanza asiye Mnigeria kupokea heshima.

Ali Kiba ametajwa kama msanii mwenye mafanikio akiwa na zaidi ya miongo miwili ya mafanikio, msanii huyo amejidhihirisha kama mwanzilishi wa miondoko ya muziki wa Bongo Fleva.

Akizungumzia tuzo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa tuzo za NXT Honors Saliu Momoh, alimpongeza Alikiba kwa mchango wake katika muziki wa wake.

“Mchango wa Ali kiba katika muziki wa Afrika unazidi nyimbo zake. Amekuwa nguvu ya kiutamaduni, akiziba pengo kati ya bara lote la Afrika huku akibaki mwaminifu kwa mizizi yake. Ni haki tumtambue kwa urithi wake kwa heshima yetu ya juu kabisa.”

“Uwezo wake wa kuchanganya midundo ya jadi ya Kiswahili na sauti za kisasa umebadilisha muziki wa Afrika Mashariki na kumweka kama balozi wa kimataifa wa utamaduni wa Tanzania, akiwa na nyimbo zisizopitwa na wakati ambazo zimegusa vizazi mbalimbali. King Alikiba anaendelea kuhamasisha mashabiki kote barani Afrika na duniani.”amesema

Mwaka 2023, Tuzo ya Heshima ya Maisha ilitolewa kwa mtayarishaji wa muziki wa Nigeria, Don Jazzy kwa mchango wake katika muziki wa Afrobeats. Kutambuliwa kwa Ali kiba ni hatua muhimu, kwani NXT Honors inaendelea kusherehekea vipaji tofauti vinavyounda simulizi la kiutamaduni la Afrika.

NXT Honors 2024/2025 itatangaza orodha kamili ya washindi katika muziki, filamu, mitindo, na ubunifu baadaye mwezi huu.

Related Articles

Back to top button