Burudani

Abby Skills Muziki ulinipa fedha lakini sikuwekeza

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva Abby Skills amesema utoto ndiyo uliosababisha ashindwe kumalizia ujenzi wa nyuma yake licha ya kupata fedha nyingi katika muziki wake.

Msanii huyo alisema wimbi wake wa Nakupenda aliouimba na Dully Sykes na Zahran ulimuingizia fedha nyingi lakini hakuwekeza kwenye shughulinza uzalishaji.

“Kipindi kile nilikuwa nikipata fedha nyingi kutokana na shoo za nchi mbalimbali na mikoani lakini ilikuwa ni utoto mwingi nilijiona na pesa nyingi chakufanyia sikukiona nimesafiri maeneo mengi nimetengeneza fedha nyingi lakini nilifanya mambo ya ujana,” alisema Abby Skills.

Anasema wimbo wa Avelina ndiyo ulimpa akili ya kuwekeza katika ujenzi wa nyumba ambayo badi haijaisha.

“Nilinunua gari, nguo na vitu mbalimbali vya kidunia nikajua ntapata fedha za kumaliza nyumba lakini sikufanikiwa kumalizia,” alisema.

Related Articles

Back to top button