Burudani

Yemi Alade, Femi One, Mjamaica waachia ‘Baddie Remix’

LAGOS: MWIGIZAJI wa Afropop aliyeteuliwa katika tuzo za Grammy, Yemi Alade ametoa wimbo wake mpya wa ‘Baddie’ ambao amewashirikisha Femi One kutoka Kenya na msanii Konshens kutoka Jamaica.

Ushirikiano huo uliotolewa chini ya Kundi la Muziki la Effyzzie unaunganisha Afrika na Karibea, kupitia mchanganyiko wa Afrobeats, Hip Hop na Dancehall.

Video ya wimbo huo imechukuliwa Kenya na Miami, muongozaji wa video hiyo ni mtengenezaji wa filamu aliyeshinda tuzo za Ovie, ameufanya wimbo huo kuwa na mvuto utakaopendwa duniani kote.

Wimbo huo umechanganya mandhari ya jiji na vipengele vya kitamaduni na uzuri wa kisasawa maeneo hayo ikionyesha zaidia utamaduni na muziki wa afrika.

Katika wimbo huo baada ya Yemi Alade kuimba utasikia maneno ya rapa mkali wa Kenya Femi One makali yenye mvuto kuyasikiliza huku Konshens wa dancehall akiingiza ladha yake ya Kijamaika.

“Mimi ni shabiki mkubwa wa Konshens na tulikutana kupitia Instagram DM na tukafanya muziki mzuri na Femi one nilimtafuta kwa kuwa ni mmoja wa ma MC ninaowapenda wa kike. Nimefurahi tumetengeneza remix hii.”

Femi One aliongeza, “Kuwa sehemu ya ‘Baddie Remix’ ni hatua muhimu. Kushirikiana na Yemi na Konshens imekuwa ndoto na ninafuraha kwa ulimwengu kusikia tulichofanya. Huu ni zaidi ya wimbo wenye msisimko mno!”

Konshens naye amedai kwamba, “Remix hii ni moto! Ni heshima kwangu kuwa katika wimbo mmoja na wakali wawili wa Kiafrika. Yemi na Femi kwa pamoja tumeunda ‘banger’ ambayo inawakilisha ubora zaidi wa Afrika.”

Yemi Alade ni mshiriki wa tuzo za Grammy 2025 zitakazo fanyika Februari 2, kupitia wimbo wake wa ‘Kesho’ uliotoka katika albamu yake ya ‘Rebel Queen’ ambayo ndiyo iliyoutambulisha wimbo uo mpya wa ‘Baddie Remix’.

Related Articles

Back to top button