
DAR ES SALAAM: Mkurugenzi wa Masoko wa Startimes Media David Malisa amezindua kampeni ya msimu wa sikukuu ya Lipa Tukubusti kutoa nafasi kwa wadau wa michezo, burudani na Jamii kunufaika na huduma zao mbalimbali.
Startimes ni miongoni mwa makampuni yaliyodhamini michezo ikiwemo Ligi ya Championship na imekuwa ikitoa fursa kwa wasanii mbalimbali wa tamthiliya kuonesha kazi zao lakini pia, wakirusha matangazo ya Mpira wa Ulaya’ na tamthiliya za kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Malisa amesema wameona walete kampeni hiyo msimu huu wa sikukuu kwa kuwa wengi wako likizo majumbani hivyo watapata fursa ya kufuatilia vipindi vyao vya burudani kwa umakini mkubwa kwa bei nafuu.
“Lipa tukubusti tunamaanisha kuwa utakapolipia kila kifurushi tutakupandisha kwa mfano ukilipia Nyota utapanda hadi Mambo, ukilipia Uhuru tutakuongeza siku tano bure kabisa lengo ni kuendelea kuwahamaisha wadau wetu wa burudani kunufaika na wengine kuingia katika familia,”amesema.
Pia, amesema pamoja na kampeni hiyo Kuna Chanel mpya zimeongezwa ikiwa ni pamoja na ya watoto, discovery na Kuna tamthiliya mpya za kimataifa zimeongezeka.
Kwa upande wake, Mkuu wa Maudhui tv3 Emanuel Sikawe amezungumzia kuhusu Ligi ya Championship kuwa tayari wamerusha mzunguko wa kwanza na sasa wanatarajia kurusha mzunguko wa 12 mwishoni mwa wiki hii.
Alisema lengo ni kuwafikia wadau mbalimbali wa michezo na kuvionesha vipaji vya soka kuanzia ngazi ya chini.
Naye Mkuu wa Maudhui Chanel ya St Bongo Shikunzi Haonga alisema wanajivunia ndani ya Startimes wanatarajia kuja na msimu mpya wa onesho la Mr Rights wiki ijayo.
Alisema onesho la kwanza la shindano hilo litarushwa kuanzia Desemba 2, mwaka huu .