Filamu

Kate Winslet afichua yaliyofichika katika filamu ya Titanic

NEW YORK: BAADA ya miaka mingi kupita na filamu ya Titanic kufanya vizuri katika mauzo duniani kote ambapo inashika nafasi ya pili kwa mauzo kwa muda wote ikifikisha dola 2bilioni lakini muigizaji wa kike katika filamu hiyo Kate Winslet amefichua kwamba kuna tukio muhimu katika filamu hiyo halikurekodiwa walipokuwa katika bahari ya Atlantiki.

Kate Winslet amesema kuwa James Cameron hakuingiza matukio muhimu waliyoshoti kwenye maji wakati wa upigaji picha za Titanic katika Bahari ya Atlantiki.
Tukio analozungumzia Kate ni lile ambalo Rose, anaonekana akielea kwenye maji akiwa juu ya mlango ulioachwa kutokana na meli kuzama, anasema eneo hilo waliigizia katika pipa lililokuwa na nafasi ndogo kupenya kwa Leonardo DiCaprio ambaye ameigiza kama Jack katika filamu hiyo.

“Tulishoti katika mazingira magumu na ilitumia muda mrefu na muongozaji James Cameroon alitumia gharama kubwa sana kuandaa filamu hiyo inayofanya vizuri zaidia duniani katika mauzo na imeshinda tuzo nyingi. Mara kwa mara kulikuwa na mvua na eneo tuliloigizia kama bahari lilikuwa na hatari kubwa maana lilikuwa ni tank lenye tundu dogo ambalo kama hukutumia ujuzi binafsi wa kuogelea unaweza kuhatarisha maisha yao,” alisema Kate Winslet.

Related Articles

Back to top button