Filamu

Waziri India ataka wanawake walindwe kwenye filamu

KERALA: WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Wanawake na Watoto Jimbo la Kerala na Mjumbe wa Bunge la Kerala nchini India, Veena George amesema sekta ya filamu inapaswa kuwa mahali salama na rafiki kwa wanawake.

Waziri George amesema jukumu la usalama huo ni la mtayarishaji wa filamu husika ndiye anapaswa kuhakikisha usalama kwa watu wote anaofanya nao kazi lakini kwa upendeleo, mwanawake anatakiwa alindwe mno.

Waziri huyo ameeleza hayo alipokuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya mafunzo iliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Wanawake na Watoto, kwa ushirikiano na Gender Park, ili kuongeza ufahamu kuhusu Sheria ya POSH miongoni mwa wale wanaofanya kazi katika sekta ya filamu.

“Wanawake wanapaswa kupiga hatua. Filamu inapotengenezwa, ni muhimu kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa salama kwa kila mtu anayehusika katika sekta hii, kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya POSH 2013 na mapendekezo ya ripoti ya Kamati ya Haki Hema,” ameeleza Waziri huyo.

“Mtayarishaji anachukuliwa kuwa mwajiri na hivyo kuwa jukumu lao kuunda Kamati za ndani na kuhakikisha usalama wa wanawake mahali pa kazi. Ushiriki wa mashirika mbalimbali unaonyesha kuwa tasnia ya filamu inakubali mpango huu kwa asilimia kubwa,” George amesema.

Waziri George amesema kuwa katika mpango huo ambao takriban wanachama 60 wa tasnia ya filamu wameshiriki utakuwa bora zaidi na utaifanya tasnia ya filamu ya ‘Kimalayalam’ kuwa rafiki zaidi kwa wanawake kwa sababu pia serikali inaweka umuhimu mkubwa katika kuhakikisha usalama wa wanawake katika maeneo ya kazi.

Hafla hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu Sharada Muraleedharan, Katibu Mkuu Idara ya Maendeleo ya Wanawake na Watoto Dk Sharmila Mary Joseph alitoa hotuba ya makaribisho, huku Muongozaji filamu Haritha V Kumar akitoa shukrani.

Related Articles

Back to top button