Muziki

“Kaeni mkao wa kula, Malkia anakuja

DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Fleva Ali Kiba amesema mashabiki wake wa Kings Music wakae mkao wa kupata burudani hivi karibuni kwani anatarajia kumtangaza Queen wa Kings Music.

“Ni kweli nimekuwa nikisema mara kwa mara nitamtambulisha Queen wa Kings Music, yupo na amesharekodi tayari tulikuwa tunamalizia kwanza mambo ya Crown Tv na kinachofuata sasa ni kumtambulisha.

“Niwaambie tu wasanii wa kike wajipange, msanii wangu yupo vizuri sana. Nisiongee sana, nitakapomtambulisha wenyewe mtajionea. Yupo tayari na nyimbo zake zipo tayari hivyo mashabiki wajipange”, amesema Alikiba

Pia ameongeza kuwa kuhusu kuimba na wasanii wake ameshaimba nao kazi zinatoka zitatoka  kwa foleni.

Related Articles

Back to top button