Muziki

Ariana Grande: ‘Thank U, Next’ Iliokoa maisha yangu

NEW YORK: NYOTA wa muziki wa pop mwenye miaka 31, Ariana Grande ameweka wazi kwamba alipitia wakati mgumu akipambana na ugonjwa wa mfadhaiko (PTSD) kufuatia shambulio lililotokea wakati wa tamasha lake katika ukumbi wa Manchester Arena mwaka 2017 ambapo watu 22 walifariki na watu zaidia ya elfu moja kujeruhi.

Mwanamuziki huyo amefichua kuwa kufanyia kazi albamu hiyo ilikuwa ni aina ya tiba kwake baada ya kukumbwa na janga hilo.

Wakati akihojiwa kwenye podikasti ya The Hollywood Reporter’s ‘Awards Chatter’, Grande ameeleza: “Nilikuwa nikifanya tiba nyingi, na nilikuwa nikishughulika na PTSD na aina zote tofauti za huzuni na wasiwasi.

“Kwa kweli, nilikuwa nikiichukulia kwa uzito sana, lakini albamu hii nilipokuwa nikiifanya ilikuwa sehemu ya tiba iliyochangia kuokoa maisha yangu. Zilikuwa nyakati za giza, na muziki ulileta hali ya juu sana.”

Ariana aliyetamba na wimbo wa ‘Sweetener’amefichua kwamba uongozaji wake hawakushawishiwa na mpango wake wa kuzindua albamu nyingine mara tu baada ya ile ya mwisho.

Grande aliongeza: “Lebo ilielewa kuwa nilihitaji kuachilia ‘Thank U, Next’, lakini pia walisita sana kuacha wimbo wa ‘Sweetener’ hivyo wimbo huo ukaingizwa kwenye albamu…

“Sijali sana kuhusu fomula. Sitaki kufuata sheria za kampuni kwa wakati huu, kwa sababu hiki ndicho ninachohitaji kwa ajili ya nafsi yangu. Nahisi uponyaji na uhuru wa kweli.”
Hata hivyo baada ya kubadilisha sauti yake ili kulinda sauti yake kwa miaka ijayo Ariana Grand amekabiliwa na ukosoaji wa juu mitandaoni kutokana na kubadilisha sauti yake ambayo kwa sasa anazungumza kwa juu zaidi kuliko hapo awali, lakini Ariana mwenyewe anasisitiza kuwa hajali kwa kuwa anafanya hivyo kwa ajili ya manufaa ya sauti yake.

Related Articles

Back to top button