Muziki

Kikwete kuwa mgeni rasmi tamasha la kuombea uchaguzi mkuu

Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Uimbaji na Maombi ya kuombea Uchaguzi Mkuu, lililoandaliwa na Kwaya ya Zabron Singers. Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Aprili 13 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Akizungumza na Spotileo, Katibu wa Zabron Singers, Emmanuel Zabron, amesema tamasha hilo lijulikanalo kama Mkono wa Bwana Blessing litatoa fursa kwa waimbaji wachanga wa nyimbo za Injili kumsifu Mungu na kuombea taifa kuelekea uchaguzi mkuu.

“Tunapokaribia kipindi muhimu kwa taifa letu, tunawaalika waumini wote kushiriki nasi katika tukio hili la kiimani na kijamii kwa ajili ya kuliombea taifa letu,” amesema Emmanuel Zabron.

Aidha, ameeleza kuwa tamasha hilo pia ni sehemu ya kukuza vipaji vya vijana wa Afrika Mashariki ili wawe na ushawishi mkubwa katika muziki wa Injili na maisha yao ya kiroho.

Mbali na hilo, Emmanuel amesema kuwa fedha zitakazopatikana kupitia tamasha hilo zitatumika kuanzisha kituo cha huduma za jamii kwa lengo la kuhamasisha vijana kutumia vipawa vyao katika kutangaza neno la Mungu.

Related Articles

Back to top button