Muziki

John Legend amsamehe Mama yake

NEW YORK: MWANAMUZIKI wa kibao cha ‘All of Me’ ameweka wazi namna alivyomsamehe mama yake Phyllis aliyekuwa akitumia dawa za kulevya.

Akizungumza kwenye ‘The Lulu Podcast: Turning Points’, Legend amesema: “Haikuwa rahisi kumsamehe mama… kimsingi tulimpoteza mama yetu kwa muda alipokuwa akipambana na uraibu baada ya mama yake kufariki.

“Kwa hivyo alikuwa nje ya maisha yetu kwa muda… ilitufanya tujihudumie na kujitegemea wenyewe…
“Tulipokuwa watoto wadogo tulikuwa tunapika na kufanya kazi za nyumbani wenyewe kwa kuwa mama aliondoka katika maisha yetu.”

Mwimbaji huyo mwenye miaka 46 amesema alipokuwa kiumri akatambua kuwa mama yake alikuwa akitumia dawa za kulevya hivyo: “Nikatambua kuwa unaposamehe huwa unasamehe kwa ajili ya nafsi yako mwenyewe … njia bora ya kila mtu kupona ni kusamehe.”

Amesema: “Tukiwa wadogo tunawakasirikia wazazi wetu tukitazamia wawe wakamilifu na wafanye mambo yote yanayotufaa, lakini tukikua kiumri tunatambua kwamba wao ni binadamu kama sisi.”

John Legend na mkewe Chrissy Watoto wao ni Luna, wanane, Miles, sita, Esti, wawili, na Wren ambaye anamiezi sita kwa sasa.

Related Articles

Back to top button