Muziki

Diamond Platnumz aachia kionjo cha albamu Mpya

DAR ES SALAAM: MKALI wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amezua gumzo kwa mashabiki wa muziki huo baada ya kutangaza albamu yake ijayo inayotarajiwa kuachiwa mwezi ujao.

Kwenye mtandao wa Instagram, msanii huyo amedokeza juu ya albamu hiyo ambayo hajaitaja jina lake.

“Albamu ya Bongo Fleva kabla ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani,” aliandika kwa mamilioni ya wafuasi wake na kudokeza zaidi; “Sahau Zuwena. “Yatapita ni takataka tu,” aliandika kwa ujasiri, akinadi albamu hiyo kwamba ina nyimbo bora zaidi ya nyimbo zake zilizopita.

Kwa miaka mingi, ushirikiano wake wa kimataifa umemuimarisha zaidi Diamond Platinumz kisifa na kiubora pamoja na kuinua usanii wake.

Toleo kuu la mwisho la Diamond, ‘A Boy From Tandale’, iliachiwa mnamo 2018, na kufuatiwa na EP ya Kwanza mnamo mwaka 2022.

 

Related Articles

Back to top button