Mshindi wa Grammy, Tyla atangaza albamu yake mpya ‘Deluxe’

JOHANNESBURG: MWIMBAJI maarufu wa muziki wa Pop kutoka Afrika Kusini, Tyla anajiandaa kuachia toleo jipya la albamu yake ya kwanza Ijumaa hii.
Msanii huyo aliingia kwenye mitandao ya kijamii na kuweka chapisho lake: ‘TYLA (Deluxe) Ijumaa hii Oktoba 11. Pamoja na tangazo hilo, ameorodhesha baadhi ya nyimbo mpya zitakazojumuishwa katika toleo hilo kuwa ni ‘Shake Ah’, ‘Push 2 Start’ na ‘Back to You’.
Akitokea Johannesburg, Tyla alitoa albamu yake ya kwanza Machi 22, 2024, yenye nyimbo kali kama vile ‘Water’, ‘Truth or Dare’, ‘Art’ na ‘Jump’. Katika albamu hiyo amewashirikisha wasanii nyota wa kimataifa akiwemo ‘Tems’, ‘Travis Scott’, ‘Skillibeng’ na ‘Gunna’.
Miongoni mwa sifa zake nyingi, Tyla alishinda tuzo ya Grammy ya Maji katika kipengele cha Utumbuizaji Bora Afrika.