Janet Jackson aomboleza kifo siku ya kuzaliwa kaka yake
CALIFORNIA: DADA wa aliyekuwa mwanamuziki kutoka Marekani Tito Jackson, Janet Jackson ametoa ujumbe wa kuomboleza siku ya kuzaliwa kwa kaka yake huyo Oktoba 14, 2024 ambayo ndiyo siku yake ya kuzaliwa ambapo kama angekuwa hai angetimiza miaka 71.
Janet mwenye miaka 58 na wafuasi milioni 20.8 kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ameeleza mitandao kadhaa nchini Merekani kwamba amemkumbuka kaka yake siku ya kuzaliwa kwake kwani kama angekuwa hai angetimiza miaka 71.
‘Upumzike kwa amani milele. Ninakukumbuka sana!’ alieleza Janet.
Tito ambaye alikuwa kwenye kundi la muziki la Jackson 5 alifariki Septemba 15 kutokana na mshituko wa moyo katika hospitali ya New Mexico wakati aliposafiri kutoka California kwenda Oklahoma.
“Tumemaliza kula bata mzinga na kuku, kucheka na kuzungumza,” Janet alisema huku akifafanua namna Tito alivyokuwa akilalamika kuumwa kifua wakati alipokuwa akisafiri kwa njia ya barabara.
“Tulikuwa tukicheza na mvua ilipoanza kunyesha. Hapo ndipo Tito aliporudi kwenye dirisha la upande wa abiria na kusema, “Kifua kinaniuma”
“Sijisikii vizuri kifuani mwangu.” Alijifuta uso, akavua shati lake na ilikuwa kama mtu amemtupia ndoo ya maji.” Alieleza Janet akikumbuka nyakati walipokuwa na kaka yake huyo.