Mastaa

Chino amtaja Marioo mafaniko yake

Msanii bora chipukizi kwenye Tuzo za Tanzania Music Awards ‘TMA’, Isaya Michael ‘Chino’ ameweka sawa kuhusu kuacha kumtaja staa wa muziki Omary Mwanga ‘Marioo’ kama moja ya watu wenye mchango kwenye safari yake ya Music.

Akizungumza kwenye mahojiano na moja ya redio nchini, Chino amesema alikuwa na furaha ya kupitiliza .

“Nilikuwa na furaha sana ile siku ndio maana sikumaliza maneno yote kuna baadhi ya maneno nilikosea kwa furaha, Kuna watu wengi sikuwataja kama kina S2kizzy lakini sipendi kutengenezewa stori,”

“Mimi ni kijana ninaepambana na nina mchango kwa wasanii kibao sio lazima niwe naongea Ukizingatia Marioo na mimi ni mkubwa kuliko yeye nimezaliwa 1995 lakini tulianza kazi tukiwa tunapambana hatuna kitu kwahiyo wote tumesaidiana kwahiyo hata Marioo anapaswa kunishukuru,”

“Nimekutana na Marioo mimi tayari nilikuwa dansa wa msanii Rich Mavoko najulikana nimewahi kucheza mpaka wasafi, RichMavoko ndio amefanya watu wanijue, “amesema Chino

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button