Mastaa

Fumanizi lamkatisha tamaa ya mahusiano Mimi Mars

DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo Fleva nchini Marianne Mdee, ‘Mimi Mars’ amesema kuwa ameshawahi kukata tamaa kwenye mahusiano baada ya kuvunjika kwa mahusiano kadhaa, ‘Break Up’ ikiwemo aliyowai kumfuma mpenzi wake aliye muamini sana na mwanamke mwingine.

Mimi Mars amesema alimuacha mpenzi wake huyo na Kwenda chuo kusoma alipofika alikuta masomo yamehairishwa na kuamua kurudi nyumbani alipokuwa amemuacha mpenzi wake.

“Niliporudi nilimkuta mpenzi wangu yupo na mwanamke mwingine katika nyumba tunayoishi  kitu ambacho kilinishangaza na aliponiona aliniuliza kuwa wewe siulienda chuo mbona umewai kurudi nyumbani kuna nini?

“Japo nina maumivu kwa uchungu yaani nimemkuta na mwanamke mwingine bado ananiuliza nikamwambia masomo yamehairishwa nikaondoka zangu nikwaacha niliumia sana tangu hapo sikutaka tena kuendelea na mahusiano nae.”

Amesema kuna hali ukiona huielewi kwa mwenzako unaweza tu ukakaa pembeni husipambane kwa mtu ambaye hana muda na wewe.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button