Muziki

Heavenly Voice Gospel Band waanika mipango yao

BENDI inayokuja kwa kasi kwenye muziki wa Injili, Heavenly Voice Gospel Band yenye makazi yake nchini Marekani imeweka wazi mipango yake ya kuwahudumia mashabiki.

Akizungumza na Spoti Leo Mwanzilishi na mwalimu wa bendi hiyo, Maisha Manase, amesema baada ya Mungu kumpa maono ya kuanzisha Heavenly Voice Gospel Band, ameanza mipango ya kuwafikia mashabiki wengi ulimwenguni kote.

“Kuna msemo unasema ‘follow you’re dream’ nilifatisha ndoto zangu, niliona nikiunganisha timu kama hivi kwa pamoja wengi wanaweza kubarikiwa na sasa tumeanza kukimbiza ndoto zetu za kumtumikia Mungu.

“Japo kuwa changamoto ni nyingi hasa za kifedha pale tunapoalikwa kwenye huduma mbali na nyumbani, hivyo tunamuomba Mungu atuinulie watu watakaotubeba kwenye hilo,” anasema Maisha.

Akizungumza na Spoti Leo, msemaji wa Heavenly Voice Gospel Band, Brazzoff Mwibelecha, amesema tayari wana nyimbo nyingi na wanajiandaa kufanya live recoding hivyo mashabiki wakae tayari.

“Kundi hili la sauti ya mbinguni ina mambo mengi sana, kwa msaada ya Mungu tumejiandaa vya kutosha kwa nyimbo nyingi zenye upako, muhimu ni sapoti yako maana bila hivyo hatuwezi kufika mbali,” amesema Brazzoff.

Aliongeza kwa kutaja baadhi ya waimbaji wachache kwenye bendi hiyo kuwa ni Rachel Saleh ambaye ni kiongozi wa nidhamu, Mao Kakozi ambaye ni kiongozi wa muziki (Music Director), Vyizigiro Emelina, Tuyishime Sifa, na Christina Niyo wakiwa ya chini ya Mchungaji Kiongozi Dk Vitalis Kyulule.

Related Articles

Back to top button