Muziki

Budju aibuka na wimbo mpya ‘Safe In You’

DAR ES SALAAM: STAA wa muziki wa Injili anayeishi Canada, Jonathan Budju, amewataka mashabiki wake wakae tayari kwa ajili ya ujio wa wimbo wake mpya unaoitwa Safe In You, unaotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Msanii huyo ambaye alifanya vizuri kwenye chati za muziki wa Injili kupitia wimbo wake wa sifa zake,  amekamilisha maandalizi ya kazi yake mpya yenye audio pamoja na video.

Akizungumza na SpotiLEO ujio wa wimbo huo, Jonathan amesema kuwa Safe In You utaachiwa rasmi Machi 27 kupitia majukwaa yote ya kidijitali, huku pia ukitarajiwa kuanza kuoneshwa kwenye vituo vikubwa vya televisheni Afrika Mashariki na Kati.

“Niliachia EP mwezi Januari ambayo imefanya vizuri sana kwenye mitandao. Nawashukuru mashabiki wangu na nawaomba waendelee kuwa tayari kupokea Safe In You, wimbo wenye ujumbe wa nguvu za Mungu utakaowabariki wengi,” amesema Jonathan.

Related Articles

Back to top button