Taylor Swift ndiye mwanamuziki wa kike Tajiri zaidi duniani kwa sasa

NEW YORK: MWIMBAJI wa Marekani Taylor Swift sasa amemtoa mwanamuziki na mrembo Rihanna katika nafasi ya kwanza kama mwanamuziki tajiri zaidi wa kike duniani.
Licha ya kuongoza kwa wasanii wa kike lakini utajiri wake kwa jumla Taylor Swift anashika nafasi ya 2,117 kwa utajiri zaidi duniani, kulingana na Forbes huku Rihanna akishika nafasi ya 2,336.
Kulingana na Forbes, Swift, ambaye alifikia hadhi ya bilionea mwishoni mwa mwaka jana, alipata ongezeko la thamani kutokana na mafanikio yake ya ziara ya Eras, Swift anashikilia rekodi ya utajili mkubwa zaidi kuwahi kutokea.
Anaingiza zaidi ya dola bilioni 2 kwa ajili ya ziara hiyo. Maonyesho 125 yaliyoingiza takriban dola milioni 16 na aliingiza bilioni 2 kwa kila onyesho.
Mwimbaji huyo wa ‘Bad Blood’ sasa ana thamani ya wastani wa dola1.6 bilioni yuko nyuma ya Jay-Z, ambaye ndiye mwanamuziki tajiri zaidi duniani mwenye utajiri wa dola bilioni 2.5.
Mbali na utalii, ongezeko la utajiri wa Swift pia linatokana na orodha yake kuwa na thamani ya dola milioni 600, dola milioni 600 za ziada za mrabaha na takriban dola 125 milioni, katika mali isiyohamishika kutoka kwa nyumba zake nyingi kote Marekani, Forbes iliripoti.
Filamu yake ya ‘Eras Tour’ pia ilifanikiwa, na kujikusanyia zaidi ya dola261 milioni tangu ilipoonyeshwa kwa mara ya kwanza Oktoba 2023.
Swift alitengeneza vichwa vya habari baada ya kutangaza kuwa angerekodi upya albamu zake zote za zamani ili aendelee kubaki na sifa, umahiri na malipo ya muziki wake.
Tangu wakati huo, utayarishaji wake wa nyimbo za ‘Taylor’s Version’ umefanikiwa. “Nadhani wasanii wanastahili kumiliki kazi zao,” alisema katika mahojiano ya 2019 Good Morning America. “Ninahisi tu kwa shauku sana juu ya hilo.”
Aliyewahi kushikilia taji la mwanamuziki tajiri zaidi wa kike duniani alikuwa Rihanna. Rihanna hajatoa albamu kwa takriban muongo mmoja tangu mwaka 2016.
Hata hivyo, albamu yake ya 2007 ‘Good Girl Gone Bad’ imetumia miaka mitatu kutamba kwenye Billboard 200.