Mastaa

Hatma ya Justin Timberlake kujulikana kesho

NEW YORK: HATMA ya mwanamuziki Justin Timberlake aliyekamatwa huko Sag Harbour, New York, mwezi Juni kwa madai ya kuendesha gari huku akiwa amelewa itajulikana kesho, Septemba 13 wakati kesi yake hiyo itakaposikilizwa Mahakamani.

Wakili wake na waendesha mashtaka wameripotiwa kufikia makubaliano ambayo yataondoa shitaka la awali ambapo mkali huyo wa wimbo wa ‘Mirrors’ amekubaliana na hilo huku akisubiri uamuzi wa Mahakama.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 atapewa adhabu kwa Kwenda kinyume na sheria za uendeshaji gari nchini Marekani huku vyanzo vya habari mbalimbali nchini humo ziliieleza TMZ kwamba Justin atatakiwa kulipa faini ya dola 300 hadi dola 500 kwa kosa hilo.

Lakini Mahakama itakayosikiliza shauri hilo ambalo halijaainishwa kama aliendesha gari akiwa amelewa itaweka kiasi halisi kinachotakiwa na hakimu wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo kesho Ijumaa Septemba 13, 2024, wakati ombi hilo litakaposikilizwa.

Pia sheria ya nchi hiyo inaeleza kwamba kwa kosa hilo mwanamuziki na muigizaji huyo bado atafungiwa leseni yake ya udereva katika jiji la New York kwa mwaka mzima baada ya kukataa kupimwa na kifaa cha kutambua kama alikuwa ametumia kilevi wakati alipokamatwa na polisi.

Kesi hiyo ilivyosikilizwa awali wakili wake Justin, Edward Burke Jr, alikanusha shitaka hilo na aliomba kesi hiyo itupiliwe mbali, alidai kuwa makosa yalifanywa na afisa aliyemkamata.
Kabla ya kukamatwa kwake, mwimbaji huyo alifurahia chakula cha jioni na marafiki zake huko The Hamptons nae neo hilo lilikuwa na magari ya askari nje ya mgahawa waliokuwa wakiimarisha ulinzi.

Related Articles

Back to top button