Mastaa

Jina la Diamond Platnumz lamtisha Msanii wa Jamaika

NAIROBI: MSANII wa muziki wa reggae kutoka Jamaica, Etana ametangaza sababu zilizomfanya asitumbuize katika Tamasha la Good Vibes lililotarajiwa kufanyika, Desemba 7, 2024, akitaja kwamba hujuma za kimakusudi ndizo zilisababisha hayo.

Katika msururu wa machapisho kwenye akaunti yake rasmi ya X, Etana alifichua kwamba mtu ambaye hakutajwa jina alidaiwa kulipa kiasi kikubwa cha pesa ili kutatiza onesho lake la Nairobi.

“Kuna mtu amelipa pesa nyingi kuhakikisha onesho langu linahujumiwa! Sifurahishwi na hujuma na niweke wazi, sijitokezi kwenye shoo ya Platinumz!!!!! Yote ni nzuri!” aliandika.

Etana alidai kuwa mtu aliyehusika na madai hayo ya kuingiliwa awali aliandaa hafla tofauti na msanii wa Bongo fleva kutoka Tanzania, Diamond Platnumz katika eneo moja. Tukio hilo liliripotiwa kuahirishwa, na kupangwa tena kwa tarehe sawa na ukumbi kama wake.

“Onesho langu la Desemba 7 lilikuwa likikuzwa muda mrefu kabla ya mtu kuibuka na shoo na Diamond Platnumz siku moja na eneo moja. Kisha mara baada ya hapo, nikasikia show yao imeahirishwa,” alieleza.

Aliendelea kusema kwamba baadaye alijulishwa kwamba matukio yote mawili yasingeweza kufanyika katika eneo moja, na kulazimisha kughairiwa kwa shoo yake.

“Ghafla nasikia maonesho hayo mawili hayawezi kufanyika katika eneo moja na onesho langu usiku wa leo haliwezi kutokea. Siasa na maigizo haya yote kwa msichana mmoja. Nashangaa ni nani yuko nyuma ya yote. Kwa nini unaogopa show moja na mwanamke mmoja?” aliandika.

Tamasha hilo lililopangwa kuanza saa 7 mchana hadi saa 5:30 asubuhi, lilipangwa kufanyika katika ukumbi wa A.S.K Dome, Jamhuri Park Show Ground.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button