Hatimaye ndoa ya mwana wa bilioniea wa Asia yafungwa
MUMBAI, India: WAKATI uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu tangu mwezi machi hatimaye umewadia ambapo mtoto wa tajiri zaidi barani Asia na namba10 duniani, Anant Ambani na Radhika Merchant wamefunga ndoa katika Kituo cha Mikutano cha Jio World huko Mumbai nchini India.
Tajiri Mukesh Ambani mwenye miaka 66 ana utajiri wa dola za marekani bilioni115, kulingana na Forbes anamiliki Kampuni ya Reliance, iliyoanzishwa na baba yake mwaka wa 1966 anafanya kazi katika sekta ya mafuta ya petroli, huduma za kifedha na mawasiliano ya simu.
Tajiri huyo amewaalika watu mbalimbali na waliohuduria sherehe za harusi hiyo ni pamoja na mwanamieleka John Cena, mwanamitindo nyota Kim Kardashian, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika sherehe hiyo inayoendelea leo kwa karamu ya ‘Shubh Aashirwad’ na karamu ya ‘Mangal Utsav,’ ambayo ni ya harusi itakayofanyika kesho Julai 14 na sherehe hizo zitahitimishwa siku ya Jumatatu.
Wageni maharufu wengine walihudhuria katika harusi hiyo ni waigizaji wa filamu za India mrembo Priyanka Chopra, Nick Jonas, Rajinikanth, Mahesh Babu, Yash, Shah Rukh Khan, Salman Khan, Ajay Devgn, Vicky Kaushal, Shahid Kapoor, Ranbir Kapoor, Alia Bhatt, Katrina Kaif na Deepika Padukone.
Mtoto huyo bilionea ni mkewe muda wote walionekana kuzungukwa na marafiki pamoja na ndugu wa familia zao.
Balozi wa China nchini India, Xu Feihong, alishiriki picha za kipekee za harusi hiyo, akiwa na Anant na Radhika wakielekea kwenye sherehe zao.
Bibi harusi mwenye umri wa miaka 29, Radhika Merchant alivalia mavazi yaliyotafsiri utamaduni wa ‘Panetar,’ utamaduni wa bibi harusi wa Kigujarati unaojumuisha mavazi mekundu na meupe na Bwana harusi Anant Ambani alionekana mkimya wakati wote akiwa amevalia sherwani ya dhahabu iliyompendeza mno huku kwa pamoja walionekana wakishangazwa na ubunifu wa wasanii Abu Jani na Sandeep Khosla.
Sherehe hizo za kifahari zilianza na sherehe za kimila mwezi machi ambapo mwanamuziki wa Pop Rihanna alitumbuiza. Justin Bieber naye alilipwa dola milioni 10 kutumbuiza siku kadhaa kabla ya harusi hiyo ya jana.
Anant Ambani ndiye mtoto wa mwisho kati ya watoto wake watatu, ambao wote wako kwenye bodi ya kampuni hiyo. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 anajihusisha na biashara ya nishati katika kampuni hiyo ya babake na yuko kwenye bodi ya Wakfu wa Reliance.