Mahusiano

Mapenzi yanamtesa Kanye West

MSANII na Mwanamitindo kutokea nchini Marekani, Kanye Omari West, maarufu kama ‘Kanye West’, anasemekana kupitia wakati mgumu kwenye maisha yake ya ndoa.

Ripoti za hivi karibuni zinasema kwamba mke wake, Bianca Censori, anaweza kumudu kutengana kwao.

Kwa mujibu wa jarida la InTouch Weekly, Ye anaogopa na anajaribu kila njia kumshawishi mke wake abadilishe nia yake.

Chanzo cha karibu na rapa huyo kilisema, “Bianca anazungumza na wanasheria na kuwambia marafiki kuwa ndoa yake na Kanye iko karibu kuisha. Anaogopa sana kwamba ameamua tayari.”

Ripoti hiyo iliongeza kuwa Kanye hawezi kustahimili kukataliwa, lakini Bianca anaonekana amechoka na tabia zake. Ye na Bianca walifunga ndoa mwaka 2022 baada ya talaka yake na Kim Kardashian kukamilika.

Hivi majuzi, wamekuwa kwenye habari kwa sababu za migogoro, ikiwa ni pamoja na vazi la wazi la Bianca kwenye Grammy Awards na kauli za Kanye za chuki dhidi ya Wayahudi kwenye X.

Related Articles

Back to top button