La Liga
Barcelona yakamilisha usajili wa Dani Olmo kutoka Leipzig

BARCELONA: Klabu ya Barcelona imekamilisha usajili wa kiungo mchezeshaji wa RB Leipzig, Dani Olmo.
Dau la Euro milioni 55 limetosha kumng’oa kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania kutoka Leipzig na kutua Barcelona, klabu ambayo alianzia soka akiwa mdogo.
Olmo anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Hansi Flick na anajiunga akiwa ametoka kwenye kiwango bora kutoka kwenye michuano ya Euro 2024.
Olmo alikuwa ni mfungaji bora katika michuano ya Euro 2024 iliyofanyika nchini Ujerumani. Anaondoka Leipzig akiwa amecheza michezo 107, kufunga mabao 17 na kutoa pasi za mabao 24