Kwingineko

Haaland kukosa mechi ufunguzi Euro 2024

NYOTA wa soka Erling Haaland atakosa mechi za ufunguzi kufuzu Euro 2024 za Norway kutokana na jeraha la nyonga.

Haaland alifunga hat-trick ya pili katika muda wa siku tano alipofunga magoli matatu wakati Manchester City ikiichakaza Burnley
magoli 6-0 katika mchezo wa Kombe la FA Machi 19.

Aliondolewa uwanjani katika dakika ya 63 na vipimo vimeonesha ana majeraha ya nyonga hivyo atakuwa nje kwa angalau wiki moja.

“Erling Braut Haaland alikuwa na maumivu kwenye nyonga yake baada ya mechi dhidi ya Burnley. Baada ya kufanya vipimo imebainika kuwa hatakuwa timamu kucheza mechi dhidi ya Hispania na Georgia,”imesema taarifa ya Norway.

Norway imefuzu kushiriki ubingwa wa Ulaya mara moja tu katika historia ya nchi hiyo mwaka 2000 na itaanza kampeni ya kufuzu dhidi ya Hispania Machi 25 kisha dhidi ya Georgia Machi 28.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button