Kwingineko

Southgate aikana Man United hadharani

MENEJA wa zamani wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate ametangaza hatarudi kwenye ukocha licha ya kuwa na taarifa za kocha huyo kuhusishwa na mashetani wekundu Manchester United

Southgate aliyeachia ngazi baada ya kupoteza dhidi ya Hispania katika mchezo wa fainali ya michuano ya Euro 2024 iliyotamatika mapema mwaka huu, amekuwa akihusishwa kutua Old Trafford, huku United ikiwa bado haijaweka wazi hatma ya meneja wao wa sasa Erik ten Hag kufuatia mwanzo mbaya wa msimu.

Akizungumza katika mkutano wa Umoja wa Vilabu barani ulaya unaoendelea jijini Athens nchini Ugiriki Southgate amejiweka mbali na tetesi hizo na kusema kuwa hatakuwa sehemu ya benchi lolote la ufundi kwa mwaka ujao

“Sitafundisha timu yeyote nina hakika na hilo, nahitaji kujitathmini na kufanya maamuzi sahihi. Unapoachia majukumu makubwa kama niliyokuwa nayo unahitaji kuupa mwili na akili muda zaidi” amesema.

Southgate aliyedumu na kikosi cha The Three lions kwa miaka 8 ameiongoza timu hiyo ya taifa ya England kwenye michuano mbalimbali mikubwa ikiwemo Kombe la Dunia la FIFA la 2018 na la 2022 michuano ya Euro 2020 na ya hivi karibuni ya nchini Ujerumani.

Related Articles

Back to top button