EPL

Guardiola amfananisha Haaland na Messi, Ronaldo.

MANCHESTER:KOCHA mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester city Pep Guardiola amesema wanaomlinganisha mshambuliaji wake Erling Haaland na magwiji wa soka Lionel Messi na Christiano Ronaldo hawakosei hasa ukiangalia namba zao.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya England jumapili ugenini dhidi ya Ipswich Town Pep amesema Haaland ni aina nyingine ya mchezaji tofauti na wakongwe hao lakini kitakwimu wanalingana.
“Erling ni aina nyingine ya mchezaji, kuna suala la namba ambalo ni lazima tuliangalie sana. Leo (Messi) kama Christiano (Ronaldo) wamekuwa wakifunga magoli kwa miaka 14, 15 idadi ya kustaajabisha ya magoli kila msimu. Kila mtu anajua Erling ni aina nyingine ya mchezaji lakini tukiweka takwimu ni kama wao tu, sijui ilikuaje kwao (Ronaldo na Messi) katika umri alionao (Haaland) lakini naona wako sawa – Amesema Pep.
Erling Haaland aliyesaini mkataba mpya wa kusalia Manchester City kwa miaka 9 na nusu hapo jana Januari 17, 2025 ni wa pili kwenye orodha ya wapachika mabao wa Premier League msimu huu akiwa na mabao 16 akimfukuzia Mohammed Salah wa Liverpool mwenye mabao 18.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button