EPL

Amorim: Tunamhitaji Maguire

MANCHESTER, England: Kocha mkuu wa Mabingwa wa zamani wa Ligi kuu ya England Manchester united Ruben Amorim amethibitisha kuwa klabu yake inafikiria kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja nahodha wa zamani wa kikosi hicho Harry Maguire.

Beki huyo wa kati ameingia kwenye miezi sita ya mwisho ya mkataba wake na United na kocha Amorim ameonesha furaha yake baada ya kutaarifiwa na uongozi klabu hiyo kuwepo kwa majadiliano ya kuongeza mkataba.

“Anahitaji kujituma zaidi, tunamhitaji sana, Maguire anapaswa kuboresha kiwango chake uwanjani na kama kiongozi. Sote tunajua anayopitia lakini timu bado inamuhitaji sana hasa wakati huu”. Amorim aliwaambia waandishi wa habari kuelekea mchezo wao dhidi ya Liverpool.

“Ukiangalia kikosi chetu, utagundua tuna njaa ya viongozi uwanjani na yeye ni kiongozi mzuri anapaswa kuwa vizuri zaidi katika eneo hilo na kuboresha uchezaji wake, sisi tunafurahi kuendelea nae” – ameongeza

Taarifa hizi zinatafsiriwa na wadau wengi wa soka kama njia ya Manchester United kunufaika na biashara ya Maguire badala ya kumuacha aondoke kama mchezaji huru.

Related Articles

Back to top button