EPL

Doku, Diaz kuikosa Chelsea kesho

MANCHESTER: WINGA wa kushoto Jeremy Doku na beki wa kati wa Manchester City Ruben Diaz hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho wa ligi kuu ya England dhidi ya Chelsea kutokana na majeruhi.

Kocha mkuu wa kikosi hicho Pep Guardiola amewaambia waandishi wa habari kuwa wachezaji hao wawili wanaungana na beki Nathan Ake na Oscar Bobb ambao ni majeruhi wa muda mrefu.

Diaz aliumia katika mchezo wao wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya PSG Jumatano huku Jeremy Doku aliyeukosa mchezo huo ataendelea kutopatikana licha ya kufanya vizuri katika mchezo walioshinda 6-0 mbele ya Ipswich Town.

Manchester City wataialika Chelsea dimbani Etihad kesho Jumamosi kuanzia saa 2:30 usiku katika mchezo ambao unatazamwa kama vita ya kugombea nafasi ya 4. Man City wakihitaji kushinda ili kuishusha Chelsea katika nafasi hiyo na Chelsea ikihitaji ushindi ili isalie hapo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button