EPL

Joao Felix arejea The Blues

Mshambuliaji Joao Felix amerudi kuitumikia klabu ya Chelsea akitokea Atletico Madrid kwa ada

inayosemekana kuwa zaidi ya Euro milioni 50.

Joao Felix amesaini mkataba wa kuichezea Chelsea mpaka mwaka 2030 huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja akiwa ameshawahi kupita klabuni hapo ambapo alihudumu kwa mkopo wa miezi 6.

Felix ni mchezaji namba nne aliyewahi kununuliwa kwa pesa nyingi zaidi katika historia ambapo Atletico Madrid ilimnunua kutoka Benfica mwaka 2019 kwa ada ya pauni milioni 126 lakini hakuweza kuonesha thamani yake uwanjani hivyo akatolewa kwa mkopo Chelsea kisha Barcelona.

“Nina furaha kurudi klabuni hapa na ninasubiri kwa hamu kuanza kucheza. Nilifurahia sana kipindi changu mahali hapa, siku zote nilitamani kurudi katika Ligi Kuu ya England”, amesema Felix.

Related Articles

Back to top button