Filamu

Grogan’s Lodge’ filamu ya kiafrika inayotamba

NAIROBI: Filamu fupi ya ‘Grogan’s Lodge’ imechaguliwa kuonyeshwa katika Tamasha la Filamu fupi la Kimataifa la Clermont Ferrand, mojawapo ya matamasha yanayoonesha filamu fupi maarufu zaidi duniani.

Filamu hiyo iliyoongozwa na Isaya Evans na Shaleen imefanikiwa kuonyeshwa Amerika Kaskazini na Kusini, Afrika, Ulaya na Uingereza.

Waongozaji wa filamu hiyo inayoelezea wanafunzi wawili wa chuo kikuu cha Kenya husafiri hadi kwenye jumba kubwa la uwindaji wakiwa na nia ya kupata kazi, lakini wanajikuta wakitumbukia katika maisha ya ukoloni yenye vurugu na giza waliharikwa kuwa sehemu ya tukio katika tamasha la filamu fupi nchini Ufaransa.

Waongozaji hao waliharikwa kwa lengo la kuifanya filamu hiyo fupi kuwa ndefu na tayari wameshaandaa rasimu ya kwanza ya ‘Ghosts of the Colony’ kwa ajili ya kuanza uandaaji wake.

Rasimu hiyo pia ilichaguliwa kwa Mpango wa Jumpstart katika Jumba la Filamu la Durban nchini Afrika Kusini, ambapo pia waongozaji hao Isaya na Sheleen waliharikwa.

Naye mtayarishaji wa filamu hiyo, Densu Moseti kwa sasa amesajiliwa katika programu ya uzamili katika Shule ya Kitaifa ya Filamu nchini Uingereza.

Mnamo Oktoba 2024, ‘Grogan’s Lodge’ ilioneshwa katika Tamasha la Filamu la Nairobi ambapo ni nyumbani kwa waandaji wa filamu hiyo iliyojizolea umaarufu mkubwa duniani kote.

Filamu yenye tuzo ya ZIFF, ‘Ardhi Yetu Uhuru wetu’, pia itaoneshwa wakati wa sherehe za kufunga Tamasha la Wiki ya Filamu la Kitale nchini Kenya.

Filamu zilizopangwa kuoneshwa Jumamosi usiku ni pamoja na ‘Boda Lov’e, ‘Wamaitha’, ‘Nusu Chokoleti Nusu Vanila’, ‘Njambi’ na ‘Ndizi Zilizopotea’, na ‘Counterpunch’.

Related Articles

Back to top button