Filamu ya ‘Ne Zha 2’ yatumia milioni 80 yaingiza bilioni 2.2

CHINA: FILAMU ya Kichina ‘Ne Zha 2’ imekuwa filamu bora ya uhuishaji iliyoingiza pato la juu zaidi kuwahi kutokea duniani ikiingiza kiasi cha dola bilioni 2.2 katika mauzo ya awali duniani kote.
Filamu hiyo, imetengenezwa kwa dola milioni 80 tu, na imeshaingiza dola bilioni 2.2 ikiifanya kuwa filamu iliyoingiza fedha nyingi zaidi kuwahi kutokea duniani kote kama zilivyofanya filamu nne tu kuwa na mauzo makubwa duniani ikiwemo filamu ya ‘Avatar’ na ‘Avengers: Endgame’, ‘Avatar: The Way of Water’ na ‘Titanic’.
Walakini, 2025 filamu inayoweza kufikia dola bilioni 2 za mauzo duniani kote na kumzidi ‘Ne Zha 2’ kwenye ofisi ya sanduku labda ‘Avatar’ ya muongozaji James Cameron: ‘Fire & Ash’, ambayo itatolewa Desemba mwaka huu.
Kwa sasa ‘Ne Zha 2’ inaongoza na dola hizo bilioni 2.2 ikifuatiwa na filamu ya Warner Bros ya ‘A Minecraft’ iliyoshika nafasi ya pili ikipata dola milioni 948 duniani kote. ‘Disney’s Lilo & Stitch’ iko katika nafasi ya tatu kwa kukusanya dola milioni 632 duniani kote.
Filamu nyingine ya Kichina imeshika nafasi ya nne ni ‘Detective Chinatown 1900’ huku ‘Captain America: Brave New World’ ikifunga tano bora.




