Filamu

Mkongwe Madona ajitupa kwenye Uigizaji

LOS ANGELES: MWANAMUZIKI mkongwe Louise Ciccone maarufu Madonna amethibitisha kurejea kwenye uigizaji baada ya kutoonekana katika tasnia hiyo kwa zaidi ya miaka 20.

Nyota huyo alionekana nchini Italy akisoma script ya kazi mpya ya tamthilia ‘The Studio’, jambo lililowasisimua mashabiki wake duniani.

Tamthilia hiyo inayorushwa na Apple TV+ imekuwa maarufu kwa kushinda tuzo nyingi nje na ndani ya Marekani.

Ujio wa Madonna katika tasnia ya uigizaji na vituko vyake vingi unatarajiwa kuongeza mvuto zaidi kwa tasnia hiyo lakini kwa fani nzima ya burudani

Related Articles

Back to top button