Africa
Gomez kukiwasha Kombe la dunia

MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Wydad Casablanca, Seleman Mwalimu ‘Gomez’ ni mtanzania pekee atakayecheza michuano ya kombe la Dunia la klabu baada ya timu yake hiyo kufanikiwa kwenda kucheza michuano hiyo.
Mwalimu amesajiliwa na Wydad AC akitokea Singida Black Stars.
Katika michuano hiyo Mwalimu anaenda kukutana na wachezaji wa klabu mbalimbali zilizofanikiwa kufuzu kucheza michuano hiyo.
Mshambuliaji huyo atakuwa sehemu ya kikosi cha Wydad AC ambacho kitashiriki michuano hiyo inatarajiwa kufanyika nchini Marekani kuanzia Juni 15 hadi Julai 13.
Wydad AC ni miongoni mwa klabu zitakazoshiriki michuano hiyo wakubwa kundi moja na Manchester City, Al Ain na Juventus.