Africa

Job: Tutawashangaza Maurtania

DAR ES SALAAM: BEKI wa kati wa Yanga Dickson Job amesema kwa sasa akili yao wanaielekeza kwenye  mchezo unaofuata ugenini wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Yanga hawakuanza vizuri hatua hiyo ya makundi baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo na kupata pointi moja kwenye mechi tatu za mzunguko wa kwanza.

Hata hivyo mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili waliuanza kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya TP Mazembe dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Baada ya ushindi huo Kikosi hicho cha Wananchi kimebakiza michezo miwili ili waweze kumaliza hatua hiyo ya makundi huku hesabu zao zikiwa ni kushinda na kupata pointi sita ili kufikisha alama 10 na kwenda robo fainali.

Job amesema, kama Wachezaji wanafurahi kupata pointi tatu dhidi ya Tp Mazembe na sasa wanafikiria kwenda kufanya maajabu ugenini dhidi ya Al Hilal kabla ya kurejea kumalizana na MC Alger.

“Zilikuwa ni pointi muhimu kwetu kuzipata dhidi ya TP Mazembe, tunashukuru Mungu wachezaji tulipambana sana na sasa akili tunahamishia kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Al Hilal kwa sababu tunahitaji kufika robo fainali.

“Tunajua mchezo hautakuwa rahisi kwa sababu wapinzani wetu wapo nyumbani, lakini sisi tunataka kwenda kusawazisha makosa tuliyofanya kwenye mchezo wa kwanza tuliopoteza nyumbani,” amesema Job.

Ushindi huo wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe umeibua matumaini mapya kwa Yanga kuelekea robo fainali kwa mara nyingine msimu huu wakiwa na Kocha wao Mkuu Sead Ramovic aliyechukua nafasi ya Miguel Gamondi.

Related Articles

Back to top button