Africa

Gamondi: Akili yetu yote mchezo wa kesho

Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya CR Belouizdad kesho utakuwa wa aina yake na timu yake inatakiwa kushinda kwa namna yoyote ile ili iweze kusonga mbele.

Gamondi amesema hayo Dar es Salaam leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo wa kundi D.

“Mchezo utakuwa mgumu na utakuwa ni mchezo wenye mbinu nyingi hasa wakati gani wa kushambulia na wakati gani wa kujilinda na tumeyafanyia kazi maeneno yote mawili na kuhakikisha tutatumia vizuri kila nafasi tutakayoipata kwenye mchezo wa kesho, amesema Gamondi”

Beki wa Yanga, Dickson Job

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake beki wa Yanga Dickson Job amesema nia yao ni kusonga mbele katika michuano hiyo.

“Kwa niaba ya wachezaji wenzangu tumejiandaa vizuri na mchezo wa kesho, mwanzo lengo lilikuwa ni kuingia hatua ya makundi baada ya muda mrefu lakini sasa lengo letu kwa pamoja ni kupambana na kusonga mbele zaidi kwa kila mchezo uliokuwa mbele yetu,” amesema Job.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Novemba 2023 Algeria, CR Belouizdad ilishinda kwa mabao 3-0.

Msimamo wa kundi D hadi sasa ni kama ifuatavyo:

#  TIMU                  P     W    D    L     F    A    GD    PTS
1.Al Ahly                 4      1    3     0    4     1     3      6

2.CR Belouizdad       4      1    2     1    4     2     2      5

3.Young Africans      4      1    2     1    5     5      0      5

4.Medeama SC        4      1     1     2    3     8     -5     4

Related Articles

Back to top button