Femi Adebayo ashinda tuzo 6 za Nollywood
LAGOS: MUIGIZAJI Femi Adebayo kupitia filamu yake ya ‘Jagun Jagun’ ameshinda tuzo sita katika tuzo za 16 bora za Nollywood zilizoangazia kiwanda cha filamu huko Ilorin, Jimbo la Kwara nchini Nigeria.
Akiwa na ushindi mara sita, ‘Jagun Jagun’ amenyakua tuzo ya Vazi Bora, Filamu Bora ya Asili, Muundo Bora wa Uzalishaji, Athari Bora Zaidi, na kubwa zaidi Mkurugenzi Bora wa Mwaka.
Femi Adebayo pia ametwaa tuzo ya Mwigizaji Bora na kuwa ushindi wake wa nne katika tuzo hiyo. Filamu hiyo imeandaliwa na muigizaji na mtengenezaji wa filamu Toyin Abraham Ajeyemi.
Tuzo ya Uhariri Bora na Skrini Bora katika usiku huo imekwenda kwa Momiwa, huku Tuzo ya Muigizaji bora Msaidizi ikichukuliwa na Mercy Aigbe kupitia filamu ya Ada Omo Daddy.
Tuzo ya waigizaji wanaochipukia imekwenda kwa Ozechi Franklin Izuchukwu na Chioma Okafor.
Washindi wengine ni pamoja na Wunmi Dada, ambaye ameshinda Mwigizaji Bora kupitia filamu ya Unknown Soja, na mwigizaji Keppy Ekpenyong, ametunukiwa tuzo ya Muigizaji Bora Msaidizi kupitia filamu ya ‘Weekend’.
Kanayo O. Kanayo amekabidhiwa Tuzo ya mafanikio maishani na Gavana wa Jimbo la Kwara AbdulRazaq AbdulRahman, pamoja na Aare Abisoye Fagade wa Taasisi ya Kitaifa ya Ukarimu na Utalii nchini humo.