Filamu

Nelly Kamwelu: Uigizaji unanilipa zaidi ya urembo

MWIGIZAJI na mwanamitindo maarufu nchini Nelly Kamwelu amesema uigizaji unamlipa zaidi kuliko shughuli zake za urembo na uwanamitindo.

Akizungumza na SpotiLEO mapema hii leo, Kamwelu ambaye ni mshindi wa taji la Miss Universe Tanzania 2011 amesema uigizaji unamlipa zaidi kwasababu ni kazi anayoifanya wakati wote na urembo ni katika muda wa ziada.

“Kuigiza imekuwa kazi yangu ya kila siku na niko chini ya mkataba wa miaka minne sasa, wakati mwingine napata dili za urembo nashindwa kuzipokea kwa sababu nabwana sana na kazi zangu za uigizaji,” amesema Kamwelu.

Mshindi huyo wa taji la Miss Southern Africa international 2011 ambaye ni mhitimu wa chuo cha uigizaji cha New York Film Academy cha nchini Marekani amesema kama kutakuwa na dili zozote za urembo na zingine atafanya ikiwa siku hiyo hakuna shughuli nza uigizaji.

“Kwa hiyo hivyo ndivyo ni navyotenganisha muda wangu kati ya uigizaji na urembo,” ameongeza Kamwelu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button