Omotola Jalade: Napumzika kigiza kwa muda

LAGOS: MUIGIZAJI maarufu wa Nollywood, Omotola Jalade-Ekeinde, amefunguka sababu ya kutokuonekana kwa muda mrefu katika filamu mbalimbali za Nigeria.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Omotola alieleza kwamba alihitaji kupumzika kutoka kuigiza ili kutafakari, kuchangamsha na kupumzisha mwili wake.
Mkongwe huyo, ambaye alianza kazi yake ya uigizaji akiwa na umri wa miaka 15, alisema kuwa kufanya kazi bila kukoma kwa miongo kadhaa kulimfanya ahisi hitaji la kupumzika na kujiimarisha.
Alisisitiza kuwa kuchukua likizo ni muhimu ili kudumisha nguvu zake za ubunifu na shauku ya ufundi wa uigizaji wake.
Mwigizaji huyo aliandika, “Najua wengi hawaelewi kwa nini mimi nimechukua muda wa kupumzika kwenye filamu kwa miaka michache, kisha nitarudi na kuigiza tena!..
“Ninaona mashabiki wakiuliza ni lini nitarudi kwenye skrini, napumzika kwanza nimefanyakazi tangu nikiwa na miaka 15, kama mimi…
“Utafanya vizuri kupumzika endapo utapumzika, utajifunza upya na utacjhaji tena akili,” alisema.
Katika hatua nyingine amekanusha tuhuma za kutoka na mume wa rafiki yake akidai kwamba picha inayosambaa alipiga na mume wa rafiki yake miaka minne iliyopita na huyo mwaname alikuwa rubani katika ndege aliyokuwa amepanda hivyo aliomba kupiga naye picha kama msanii mashuhuri.