Ligi Daraja La Kwanza
Fainali ya kibabe UEFA Super Cup

FAINALI ya UEFA Super Cup inapigwa leo kati ya Manchester City na Sevilla nchini Ugiriki.
Mchezo huo utakaochezwa na mwamuzi wa kati Francois Letexier wa Ufaransa utafanyika kwenye uwanja wa Georgios Karaiskakis uliopo kitongoji cha Piraeus, mkoa wa Attica katika mji mkuu nchi hiyo, Athens.
Fainali ya UEFA Super Cup hukutanisha mshindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na bingwa wa Ligi ya Europa.