Ligi Daraja La Kwanza

Xavi kutua Man United?

KLABU ya Manchester United imeripotiwa kumfuata Xavi Hernández kujadili upatikanaji wake baada ya kuondoka ghafla Barcelona.

Mwezi mmoja tu baada ya kubadili uamuzi wake wa kuachia ngazi, mkataba wa Xavi ulisitishwa baada ya kutoelewana na Rais wa Barca, Joan Laporta kuhusu mkakati wa uhamisho wa wa wachezaji wa klabu.

Tayari Hansi Flick ametambulishwa kuwa badala wake.

Xavi amesisitiza kwamba anapanga kupata mapumziko kabla ya kutafuta kibarua kingine lakini kwa mujibu tovuti ya michezo AS, tayari United imewasiliana naye.

United inafanya mapitio ya msimu mzima na hivi karibuni itaamua hatma ya kocha wa sasa, Erik ten Hag.

Xavi pia anaaminika kukataa maombi kutoka AC Milan na timu ya taifa ya Korea Kusini.

Inaaminika siku zijazo, Xavi huenda asifundisha tena La Liga kwa sababu hataki kushindana na Barca, hivyo kufungua milango ya kuteuliwa timu za Ligi Kuu England.

Related Articles

Back to top button