Ligi Daraja La Kwanza

Wasanii wa muziki waliofanya vizuri 2023

MWAKA 2023 unaelekea ukingoni na kila mtu analo la kujivunia lakini nikitizama kwenye
sanaa ya muziki kuna watu wanastahili sifa kwa kufanya vizuri.

Ukitaja wasanii wa muziki ni kundi kubwa, lakini zaidi nitalenga wale wasanii wa kizazi kipya. Wapo wanaochipukia na wakongwe.

Waliofanya vizuri ni hawa wafuatao.

DIAMOND
Nassibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ huwezi kumuacha katika 10 bora. Ni msanii anayejitahidi na juhudi zake zinaonekana. Ni miongoni mwa wasanii waliotoa kazi nyingi
mwaka huu lakini wimbo uliompaisha zaidi ni huo aliyoshirikishwa na Jux.

Mwingine aliimba na Kofi Olomide unaitwa Achii ambao ulitazamwa na watu milioni 21 kupitia mtandao wa Youtube. Pia, ana wimbo wa Shu wa amapiano, uliokubalika zaidi kwenye mataifa mbalimbali baada ya kuonekana ukipigwa sehemu mbalimbali za starehe.

Huu una watazamaji milioni 15 na bila kusahau wimbo wa ‘Yatapita’ uliotizamwa na watazamaji milioni 43 ndani ya miezi 11 iliyopita. Diamond ni msanii mwenye kipaji nyimbo zake zinapigwa kila mahali, ameliteka soko la Afrika Mashariki kama sio Afrika.

Amekuwa akipata shoo nyingi za nje, ameshirikishwa na wasanii mbalimbali na hiyo ni inatokana na ubora.

JUX

Jina lake kamili ni Juma Mkambala. Msanii huyu kupitia wimbo wake wa Enjoy alioshirikiana na Nassibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ hakika unaweza kusema ndio bora mwaka 2023.
Wimbo huo umechezwa na kila mtu, kuanzia watoto hadi wazee sio kwa Tanzania tu bali kimataifa.

Ni wimbo ambao umepigwa kila mahali kwenye mitaa mbalimbali, kwenye majumba ya starehe, watu wanakoishi. Kupitia mtandao wa Youtube, umetizamwa mara milioni 50 ndani ya miezi minne pekee. Kwa hiyo umeonesha kupata mwitikio mkubwa.

HARMONIZE
Rajabu Abdul ‘Harmonize’ huyu ni msanii asiyekubali kushindwa. Hupambana na wakali wengine kwa kutoa muziki mzuri. Ndani ya miezi tisa iliyopita alitoa wimbo unaitwa
Single again ambao una watazamaji milioni 25.

Ni wimbo uliochezwa ukanda wa Afrika Mashariki nan chi nyingine za Afrika, Ulaya, Asia na Marekani. Pia, miezi 11 iliyopita alitoa wimbo unaitwa Wote ambao sasa una watazamaji
milioni 10.

Ulifanya vizuri na kupokelewa vyema na mashabiki zake. Ukiacha huo, nyingine zilizofanya
vizuri ni Sijalewa, Bosi, Hawaniwezi na nyingine nyingi. Amefanya shoo mbalimbali za ndani nan je ya nchi na kuingia fedha nyingi.

ALIKIBA
Ali Salehe ndio jina lake. Mwenyewe anajiita mfalme, naweza kusema bado Alikiba anakimbizana na washindani wake. Bado anaendelea kufanya vizuri na mwaka huu alitoa
nyimbo nyingi ila baadhi zilikubalika na zilikuwa bora kwake.

Kuna wimbo wa Mahaba ndio wimbo wake bora uliofanya vizuri zaidi 2023 ukiwa na watazamaji miioni 21 ndani ya miezi 10. Wimbo wake mwingine uliofanya vizuri ni Sumu umekuwa na ujumbe mzuri na umekubalika sana mtaani.

Aliimba na Omar Mwanga ‘Marioo’ na una watazamaji zaidi ya milioni sita. Zipo nyingine
zilifanya vizuri kama Huku alioimba na Tommy Flavor, Pia, kuna wimbo wa Mnyama aliotunga maalum kwa ajili ya klabu ya Simba umefanya vizuri na kupokelewa na mashabiki.

Wimbo huu una watazamaji Milioni tatu ndani ya miezi minne.

RAYVANNY
Anaitwa Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’. Ni miongoni mwa wasanii ambao hawabaki nyuma. Amekuwa akitoa nyimbo mara kwa mara na nyingi zimefanya vizuri. Miongoni mwa nyimbo zake zilizofanya vizuri ni Forever yenye watazamaji milioni 7.8 Youtube.

Nitongoze yenye watazamaji milioni 11 akiwa amemshirikisha Diamond Plutnumz na
nyingine nyingi.

MARIOO
Omar Mwanga ‘Marioo’ ni msanii mwenye kipaji mwenye uwezo wa kutunga mashairi na kuimba. Ni kama Diamond akishirikishwa kwenye wimbo lazima uwe mzuri. Huwezi kuacha kumtaja kwa ubora na mwaka huu amefanya kazi nyingi za kwake na za kushirikishwa
na wengine.

Miongoni mwa kazi zake zilizofanya vizuri ni Love Song aliomshirikisha Alikiba ina watazamaji zaidi ya milioni tano, Sing, Shisha alioimba na Mr Nice na nyingine nyingi.

Hao wa juu ndio wanaoongoza lakini kuna wengine pia, wanafuatia kama William Lyimo ‘Bilnass’, Oscar Lelo ‘Whozu’, Barnaba Elias ‘Barnaba Classic’, Sharif Juma ‘Jay Melodies’, Shariff Ramadhan ‘Darassa’, Dulla Makabila, Sholo Mwamba na wengine wengi.

Kwa upande wa wanawake wapo baadhi wanaojitahidi kutoa nyimbo mara kwa mara na kufanya vizuri.

ZUCHU
Zuhura Othman ‘Zuchu’ ni msanii wa kike anayejitahidi sana chini ya Lebo ya Wasafi.
Miongoni mwa nyimbo zilizofanya vizuri ni Nani aliomshirikisha msanii wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Innos B, yenye watazamaji milioni 10, Utaniua yenye watazamaji milioni 15, Honey milioni 22.

Nyingine ni Naringa na Chapati ambazo zinaendelea kufanya vizuri. Amefanya shoo nyingi mwaka huu za nje na ndani ya nchi.

NANDY
Faustina Charles ‘Nandy’ ni miongoni mwa wasanii wa kike ambao huwezi kuacha
kuwataja sio kwa jinsi walivyo kwa muonekano mzuri bali ana sauti nzuri pia.
Pamoja na majukumu ya kulea aliyokua nayo, hajaacha kutoa muziki kila mara.

Kuna wimbo wake unaitwa Falling ulifanya vizuri mwaka huu ukiwa na watazamaji zaidi ya milioni tatu. Zipo nyingine kama Follow, Raha na nyingine. Wengine ni Judith Wambura
‘Ladyjadee’, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, Rosary Robert ‘Rosa Ree’, Maua Sama, Abigael Chams na wengine wengi.

Related Articles

Back to top button