Ligi KuuNyumbani

Dube: ‘Thank You’ Azam FC

MSHAMBULIAJI Prince Dube ametangaza rasmi kuondoka katika klabu ya Azam.

Katika taarifa yake Dube amewashukuru kwa dhati wote wanaohusika na klabu, kuanzia uongozi hadi benchi la ufundi, wachezaji wenzake na muhimu zaidi mashabiki.

“Kwa hisia tofauti natangaza kuondoka Azam FC. Miaka hii minne imekuwa safari ya ajabu, iliyojaa changamoto, ushindi na kumbukumbu zenye thamani,” amesema Dube.

Hivi karibu Mkuu wa Kitengo cha habari cha Azam Thabit Zakaria amesema Dube ana mkataba na klabu hiyo hadi 2026 na iwapo mchezaji huyo anataka kuuvunja lazima afuate taratibu.

Amesema klabu yoyote inayohitaji huduma ya mchezaji huyo inapaswa kukaa mezani na Azam ili kufikia maamuzi.

Related Articles

Back to top button