Ligi KuuNyumbani

Ni mtifuano KMC vs Coastal

LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa Dar es Salaam.

‘Watoza ushuru’ wa Manispaa ya Kinondoni, KMC ni wenyeji wa ‘Wagosi wa Kaya’, Coastal Union ya Tanga kwenye uwanja wa Uhuru.

KMC na Coastal zina pointi 15 na michezo 15 kila moja lakini KMC inashika nafasi ya 10 wakati Coastal ipo nafasi ya 12 kutokana na tofauti ya mabao.

Ligi kuu ilisimama baada ya raundi 15 kupisha michezo ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC).

 

Related Articles

Back to top button