Mukwala umepigaje hapo?!
KIGOMA: BAO pekee la mshambuliaji Steve Mukwala dakika ya 90+7 limetosha kuipa Simba ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma na kukwea hadi nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mukwala alipiga mpira kwa kichwa katikati ya mabeki wa Mashujaa baada ya kuunganisha kona iliyopigwa na Awesu Awesu .
Mchezo huo ulikuwa wa ushindani ndani ya dakika 90 Simba walifanya shambulizi dakika ya 20 Leonel Ateba alifanya kazi nzuri lakini Kibe Denis alipiga shuti na mpira kutoka nje.
Awesu Awesu amefanya kazi nzuri dakika 83 alipiga pasi lakini Kibu alipiga shuti na mpira ukawa mrefu na kutoka nje la lango la kipa wa Mashuja.
Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 22 na kusongea nafasi ya pili na kumshusha Singida Black Stars kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.