Ligi Kuu

Barker: Simba tuko tayari kuivaaa Pamba

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Simba SC, Steven Barker, amethibitisha kuwa kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Pamba kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Barker amesema timu iko katika hali nzuri kimwili na kisaikolojia, licha ya kuchelewa kucheza mechi iliyopita mwishoni mwa wiki. “Kutocheza mechi iliyopita kunatupa nafasi ya wachezaji kujirejesha upya, na sasa tupo tayari kikamilifu,” amesema.

Kocha huyo amesema kuwa mechi hiyo haitakuwa rahisi, kwani Pamba ni timu yenye kiwango kizuri na wachezaji wenye ujuzi.

“Nimeitazama Pamba dhidi ya Azam, walionesha kiwango bora hasa kipindi cha kwanza. Ni timu iliyofundishwa vizuri na wachezaji wake wanaweza kuleta tofauti,” amesema Barker.

Barker ameweka wazi kuwa ushindi ni muhimu sana kwa Simba katika mbio za ubingwa. “Hizi ni mechi ambazo lazima tushinde. Hakuna mechi rahisi, na hatuwezi kuruhusu kupoteza pointi,” amesema.
Kocha Mkuu wa Pamba Francis Baraza amesema wamejipanga kucheza mechi hiyo kikubwa wakijua ukubwa wa wapinzani wao ambao wako vizuri na wamekuwa na mwendelezo mzuri katika mechi zao zilizopita.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button