Tennis

Carlos Alcaraz atinga robo fainali Miami Open

MCHEZAJI namba moja wa tenisi duniani kwa wachezaji mmoja mmoja Carlos Alcaraz ametinga robo fainali ya michuano ya Miami Open baada ya kumshinda Mtaliano Lorenzo Musetti kwa seti 6-3 6-3.

Sasa mhispania Alcaraz, 20, atakutana katika nusu fainali na Grigor Dimitrov wa Bulgaria anayeshika namba 11 duniani, ambaye amemchapa bingwa wa mwaka 2021 toka Poland Hubert Hurkacz kwa seti 3-6 6-3 7-6 (7-3).

Mtaliano Jannik Sinner na mrusi Daniil Medvedev pia wamefuzu nusu fainali.

Bingwa wa Australia Open Sinner ameshinda kwa seti 6-4 6-3 dhidi ya Christopher O’Connell wa Australia, wakati Medvedev ameibuka mshindi dhidi ya Mjerumani Dominik Koepfer kwa seti 7-6 (7-5) 6-0.

Related Articles

Back to top button